728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
11 November 2012

KAULI YA LORD EYEZ, WAKILI WAKE NA NIKKI WA PILI KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI


Wakili wa Lord Eyes jana ametoa ufanunuzi kuhusu tukio lililotokea la msanii Lord Eyez kuhusishwa na tuhuma za wizi wa vifaa vya kwenye gari na kusema kuwa dhumuni la kuwaita waandishi wa habari ni kutaka Jamii itoe nafasi kwa vyombo vya sheria kutoa majibu juu ya tuhuma hizo na baada ya hapo ndipo waanze kuongelea na kwamba kwa sasa hivi kinachoendelea ni habari ambazo watu wanaozitoa hawana uhakika nazo. Wakili huyo alisema kuwa Lord Eyez hana hatia hadi pale vyombo vya sheria vitakaposema kuwa msanii huyo kweli anahusika na shutuma hizo za wizi. Kwa upande wa Lord Eyez amesema, watu wanajua kuwa yeye ni mwanamuziki kwa muda wote na hajihusishi na maswala ya wizi na ameomba mashabiki wake wavumilie kipindi hichi ambacho anapigania haki na mwishoni ukweli utajulikana....

Lord Eyez kwenye picha akizungumza na waandishi wa habari alianza kwa kumshukuru Mungu kwa kumpa nguvu katika kipindi hiki kigumu ambacho kesi ya kutuhumiwa kwake kuhusika na wizi wa vifaa vya gari ikiendelea..MSIKILIZE...alichokisema ....


Wakili wa msanii Lord Eyez Bwana Peter Kibatala akielezea tukio zima kuhusiana na Lord Eyez...MSIKILIZE akizungumzia tukio zima la msanii huyo na dhumuni la kuitisha mkutano na waandishi wa habari
 


Msemaji wa kundi la WEUSI Nikki wa Pili akizungumzia ni jinsi gani ishu ya Lord imewaathiri kundi hilo..MSIKILIZE hapo chini


Story na AnnaPeter
KAULI YA LORD EYEZ, WAKILI WAKE NA NIKKI WA PILI KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI Reviewed by Nolniz on Sunday, November 11, 2012 Rating: 5 Wakili wa Lord Eyes jana ametoa ufanunuzi kuhusu tukio lililotokea la msanii Lord Eyez kuhusishwa na tuhuma za wizi wa vifaa vya kwenye g...

Labels:

[News][carousel1]

No comments: